Pombe Si Maji, Chupu Chupu Auone Mlango wa Ahera

Go down

Pombe Si Maji, Chupu Chupu Auone Mlango wa Ahera Empty Pombe Si Maji, Chupu Chupu Auone Mlango wa Ahera

Post  Admin on Tue Nov 10, 2009 11:58 pm

Mwanamke mmoja nchini Marekani ambaye alikuwa kalewa chakari kwa pombe alinusurika sentimeta chache sana kuuona mlango wa ahera baada ya kuyumba kuyumba na kuangukia kwenye reli wakati treni likiwa karibu.
Akiwa amelewa chakari baada ya kutoka kwenye vilabu vya starehe, mwanamke mmoja nchini Marekani amenusurika chupu chupu kusagwa sagwa na treni baada ya kuangukia kwenye reli wakati treni likiwa karibu.

Mwanamke huyo alikuwa akisubiria treni kwenye stesheni ya North Boston wakati alipoanza kuyumba yumba na kisha kuangukia kwenye reli.

Abiria wengine waliokuwa kwenye stesheni hiyo walifanya kazi ya ziada kumpungia mikono dereva wa treni ili afunge breki asije akamgonga mwanamke huyo ambaye kutokana jinsi alivyokuwa amelewa sana alishindwa hata kunyanyuka na kuamua kulala kabisa kati kati ya mataruma ya reli.

Bahati nzuri treni ilisimama sentimeta chache kabla ya kumgonga mwanamke huyo huku sehemu ya mbele ya treni hiyo ikiwa juu ya mwili wa mwanamke huyo.

Mwanamke huyo alinyanyuka na kujaribu kutoka kwenye reli lakini alishindwa na kudondoka tena chari kabla ya kuokolewa na wasamaria wema.

Kweli siku hiyo haikuwa siku yake ya kifo kwani mbali ya kunusurika kugongwa na treni, mwanamke huyo alinusurika pia kuigusa reli ya tatu yenye umeme inayotumika kusambaza umeme kwenye treni.

Mwanamke huyo "Chapombe" aliondoka eneo la tukio akiwa na michubuko kwenye miguu yake.

Admin
Admin

Posts : 3
Join date : 2009-11-10

View user profile http://maishabongo.forumotion.com

Back to top Go down

Pombe Si Maji, Chupu Chupu Auone Mlango wa Ahera Empty Re: Pombe Si Maji, Chupu Chupu Auone Mlango wa Ahera

Post  masely on Thu Nov 12, 2009 12:43 am

Mkuu hii kali sana

masely

Posts : 1
Join date : 2009-11-11

View user profile

Back to top Go down

Back to top


 
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum